Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Malala Yousafzai, jana aliomba itangazwe “hali ya dharura ya elimu” nchini Nigeria, wakati alipoitembelea nchi hiyo na kukutana na baadhi ya wasichana wa shule ya Chibok.
Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 20 anayepigania elimu duniani kote alipendekeza maoni yake hayo wakati alipokutana na Makamu wa Rais Yemi Osinbajo mjini Abuja.
Nigeria ina watoto milioni 10.5 ambao hawapo shuleni – idadi kubwa zaidi ulimwenguni – na asilimia 60 ya idadi hiyo ni wasichana, kulingana na Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa , UNICEF.
