Mtandao wa polisi wanawake nchini, unatarajia kufanya sherehe za kuazimisha miaka kumi toka kuanzishwa kwake hapa nchini.
Sherehe hizo zimepangwa kufanyika tarehe 9 ya mwezi 11 mwaka huu, katika chuo cha polisi cha taaluma ya polisi Dar es salaam.
Mgeni rasmi katia sherehe hizo anatazamiwa kuwa makamu wa Rais Bi Samia Suluhu Hasani.
Antenna imeinasa sauti ya msemaji wa jeshi la polisi nchini Barnabasi David, alipozungumza na waandishi wa habari juu ya maazimisho hayo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtandao huo ACP Tulibake Mkondya, amesema baadhi ya mambo ambayo yamefanywa na mtandao huo baada ya kuanzishwa kwake.
Maazimisho hayo yanabebwa na kaulimbiu isemayo Usalama wetu ni mtaji wa maendeleo, tokomeza uhalifu kuwezesha uchumi wa viwanda.
