Mtatiro : “Sina Mpango wa Kuhamia CCM.

In Kitaifa, Siasa
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amekanusha uvumi unaonea kwenye mitandao ya kijamii kwamba ana mpango wa kukihama chama hicho na kuhamia Chama tawala cha CCM.
Kupitia taarifa yake kwa umma aliyoitoa jana  Disemba 6,2017, Mtatiro pia hana mpango wa kugombea jimbo la Kinondoni lililo achwa wazi kufuatia aliyekuwa Mbunge wake kupitia CUF, Maulid Mtulia kujiuzulu na kujiunga na CCM.
“Ndugu zangu, nimeona propaganda nyingi kwenye mitandao juu ya mimi kuhamia CCM au kuwa na mipango ya kuhamia CCM.
“Nataka niwahakikishie watanzania kuwa SIJAPANGA mipango hiyo na sina nia hiyo. Na naomba niwajulishe kuwa mtu akiwa anahamia CCM, hamuwezi kuwa na tetesi, na mimi sina kawaida ya kufanya maamuzi ghafla na kwa kujificha.
“Ningelikuwa na nia ya kuhamia CCM ningewataarifu hapa hadharani, miezi kadhaa kabla ya kufanya hivyo, walau jambo moja ambalo Mungu alinijalia ni kutokuwa mwoga na mnafiki na alinipa uwezo mkubwa wa kufanya jambo naloliamini,” alisema na kuongeza.
“Pili, nimepokea meseji nyingi sana zikiniomba nigombee ubunge jimbo la Kinondoni baada ya Mbunge wa (CUF – Lipumba), Ndugu yetu Maulid Mtulia kuhamia CCM. Nataka niweke msimamo wangu mapema, kwamba sina na sikuwahi kuwa na ndoto za kugombea ubunge wa jimbo la Kinondoni,
Masuala ya kugombea ubunge kwenye majimbo ni masuala mapana, yanahitaji maandalizi, ukaribu wako na wapiga kura na historia yako na jimbo hilo. Kwa kiasi kikubwa hakuna kigezo hata kimoja kati ya hivyo ambacho nimekikaribia, kwa hiyo sitoweza kugombea kama nilivyoona baadhi ya fikra za watu mitandaoni.”
Mtatiro amewahakikisha wanachama wa CUF kwamba anaendelea na majukumu yake ya Kamati ya Uongozi CUF, pamoja na kushirikiana na kila mtanzania kwa njia mbalimbali katika kuijenga nchi.
“Na kupitia michango yangu hiyo naendelea kuijenga Tanzania na hata kuunga mkono juhudi chanya za Rais wetu kuijenga Tanzania huku zile juhudi hasi za Rais huyo huyo hasa kwenye eneo la Demokrasia, Utawala Bora na Uchumi, nikizikemea kila siku.
“Mwisho, wapo wendawazimu wanachekelea, wanafurahia na ama kutamani vyama vya upinzani vife. Ukiona elimu ni ghali, hebu jaribu ujinga,” amesema.
Hata hivyo, Mtatiro amesema anaendelea kuwaheshimu wanaohamia CCM, kwa uhuru, utashi na mapenzi yao au kwa kununuliwa, kutokana kwamba sio wa kwanza wala hawatakuwa wa mwisho kufanya hivyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu