Kijana aliyehusika na matukio ya utekani watoto mkoani Arusha Samson Petro (18) amefariki dunia kwa kupigwa risasi na polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho alipozungumza na waandishi wa habari mapema leo.
Kamanda Mkumbo amesema kijana huyo alipigwa risasi, alipotaka kukimbia alipokuwa anakwenda kuwaonyesha polisi watuhumiwa wenzake wa utekaji, saa tano usiku wa jana
