Aliyekuwa mtendaji wa Kata ya Mwandui iliyopo mwambao mwa bonde la ziwa Rukwa, Benedict Chapewa ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi usiku wa kuamkia leo Jumatano.
Enzi za uhai wake marehemu aliwahi kuwa Katibu mwenezi wa CCM Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa jeshi la Polisi kwa sasa lipo katika msako mkali ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo pamoja na chanzo cha mauaji hayo.
