Haina maana kwamba kwenye Dunia ya leo kuwa Maarufu ni mpaka uwe mwanamuziki, au mtu yeyote ambaye anajihusisha na siasa au kazi za Sanaa.
Jamii inaweza kukupa umaarufu kwa kukuhurumia pia kwa matatizo ambayo unayapitia siku hadi siku.
Ontlametse Phalatse ni Kijana aliyetimiza miaka 18 mwezi uliopita na Jana amefariki Dunia.
Ontlametse Phalatse ni Msichana aliyejipatia umaarufu Nchini Afrika ya Kusini kwa ucheshi aliokuwa nao wa kucheka muda wote pasi na kuwaza tatizo kubwa la Maumbile lililokuwa likimtesa siku hadi siku.
Msichana huyo alizaliwa na ugonjwa uitwao Progrey Desease ambao humfanya mtu kukua haraka kupita kiasi.
Yaani mtoto mdogo lakini anaonekana kama Mzee na Mwili wake unakuwa mdogooooo ila Anazeeka ki viungo na ngozi

Mwanzoni Madaktari walisema kwamba Angefariki akifikisha Miaka 14 lakini ikawa Tofauti kwa ahadi za Mungu kwamba hakuna aijuaye kesho na Mwezi uliopita March 25 Msichana huyo alitimiza Miaka 18.
Katika siku yake hiyo ya Kuzaliwa ilitimia ndoto yake kukutana na Rais Zuma ambapo Alifanyiwa Bday Perty Ikulu ya SA na Zuma akakata naye Cake.

Amefariki usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Dr George Mukhari Academic huko Ga-Rankuwa, Pretoria.
Taarifa ya familia yake imesema: It is with great sadness to inform you of the passing of our first lady, Ontlametse Ntlami Phalatse. Our hearts are filled with pain and sadness but Ontlametse — as we know her — would want us to carry on with her courageous spirit.”
Alikuwa maarufu sana Instagram ambako alikuwa na followers 63.6k.
MUNGU AMREHEMU AMEEN!
