Mtoto Askofu Nason Ngoy aeleza mazito aliyoambiwa na baba yake kabla ya kukata Roho

Mtoto wa  mwisho wa Marehem Askofu Nason Ngoy Ngoy wa kanisa la Rehoboth lililopo kata ya Ilkiurei jijini Arusha ameeleza mazito aliyoambiwa na baba yake kabla ya kukata Roho 

Mtoto huyo ambaye ni Davison Ngoy amezungumza na radio5 mara baada ya kutembelea nyumbani kwake mianzb kata ya Ilkiurei ambapo msiba inaendelea
Amesema baba yao alifariki dunia siku ya Jumamos tar 29 usiku ambapo msiba huo ulisikilisha sana na chanzo ni kwamba alizidiwa ghafla na kupelekwa hospital ambapo madaktar walihisi ni ugonjwa wa sukari
“Tulianza kutumia dawa kwa muda wa wiki moja lakini hatukuona mabadiliko ikabidi tumeudishe tena lakini alishindwa kuongea siku ya jumatano alipona na kuendelea kufanya mazoezi, siku ya jumatano alizidiwa na kutumia mashine ya Oxygen”Alisema Davison.


Amesema kabla ya baba yake kufariki alimtaka kukaa nae karibu na kumweleza ana zawadi yake ambapo siku ya jumapili alimwita madhabahuni na kumpa zawadi ya kitabu cha kumbukumbu na biblia


Aliniambia jiandae ibadani ambapo aliniambia nipige magoti na kunipaka mafuta huku akisema Mungu amemwonyesha yeye ndo mtumishi sahihi wa kusimama kwenye madhabahu hayo akiwa hayupo na kusimamia kazi zote akiwa hayupo
“Kwangu mimi ilikuwa kama kitu cha kushtukiza na nikamwomba anipe muda lakini alikataa akaniambia nikubali au nikatae lazima nisimame badala yake na aliniambia nitakuja kuwa mtu mkubwa na kunitambulisha kwa waumini na viongozi wa kanisa kwa hiyo huu msima naona kama Mungu ndo ameuandaa” Alisema Davison
Hata hivyo Askof Dr, Ngoy Ngoy anazikwa siku ya Alhamis kwenye uwanya wa kanisa lake

http://www.radio5fm.co.tz/wp-content/uploads/2020/06/WhatsApp-Audio-2020-06-02-at-13.40.37.mp4
Sikiliza alichoambiwa Davison Ngoy na Baba yake.

Exit mobile version