Siku zote matukio ni mengi na yanashangaza yawe mazuri au mabaya antena ya Radio5fm tunakupenyezea moja inayoshangaza
Liam ni kijana mwenye miaka 10 huko Massachusetts Marekani mwezi wa sita liam alimfuata baba yake Scott Hannon na kumwambia kuwa anataka kufanya kazi ya kujitolea kwa ajili yakusaidia jamii ( community service ) alimkubalia na kushirikiana nae ili aweze kufanikisha jambo hilo .
Liam ametumia likizo yake kutengeneza mlo wa mchana kwa wale wasio na makazi na mpaka sasa liam amefanikiwa kutoa mlo 300 kwa watu hao .Tambua liam alianza kwa kutoa lunchbox 20 kwa wiki na baba ake aliamua kumsaidia kwa kuomba usaidizi kupitia GoFundMe na akafankiwa kutoa lunchbox 60 kwa wiki
Liam na baba yake wameungana na Hildebrand Family Self Help Center huko Cambridge, Massachusetts ili kupata vifaa vya shule kwa zaidi ya wanafunzi 400 ambao hawana makwao Kelly kiongozi wa maendeleo kwenye kituo hicho alidai kuwa kwa mtoto wa miaka 10 kufanya kitendo hicho cha kusaidia watu hao ni jambo lakushangangaza na la Baraka .
