Mugabe ashiriki mazungumzo ikulu Harare.

Serikali ya Afrika Kusini imesema Rais Robert Mugabe anakutana na wajumbe kutoka nchi za kanda ya kusini mwa Afrika katika juhudi za kujaribu kutatua mzozo wa kisiasa nchini humo.

Alisafiri hadi kwenye ikulu kutoka makao yake ya kibinafsi ambako amekuwa akizuiliwa na jeshi.

Wanajeshi waliingilia kati na kutangaza kudhibiti serikali Jumatano katika kinachoonekana kuwa juhudi za kumzuia mke wa Mugabe, Grace, asitwae madaraka.

Duru zinadokeza wkamba Bw Mugabe anataka kusalia madarakani hadi wakati wa kufanyika wka uchaguzi mwaka ujao.

Lakini mpinzani wake wa muda mrefu Morgan Tsvangirai amemtaka ajiuzulu mara moja kwa maslahi ya raia.

Makamu wake wa zamani Joice Mujuru pia ametaka kuwe na serikali ya mpito na pia uchaguzi huru na wa kuaminika.

Mzozo wa Zimbabwe pia unajadiliwa katika mkutano wa jumuiya ya nchi za kusini mwa Afrika, SADC, nchini Botswana.

Exit mobile version