Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, ametaka hukumu ya kifo kurejeshwa nchini humo.
Matamshi yake yanakuja baada ya afisa wa wizara ya sheria, kufichua mwezi uliopita kuwa zaidi ya watu 50 washahukumiwa kifo.
Hukumu ya kifo ilitekelezwa mwisho nchini Zimbabwe mwaka 2005, wakati mtu ambaye alikuwa akiitekeleza kustaafu kwa mujibu wa shirika la AFP.
Akiongea wakati wa maziko ya mshirika wake wa siasa kwenye mji mkuu Harare, Mugabe amesema,bora warejeshe hukumu ya kifo,sababu watu wanacheza na kifo kwa kuuana.
