Katika dakika chache zilizopita , spika wa bung la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .
Kumekuwa na shangwe miongoni mwa wabunge kufuatia tangazo hilo.
Harakati za kumuondoa madarakani rais huyo kupitia bunge kumesitishwa.habari za kujiuzulu kwake zilitolewa wakati wabunge walipokuwa wakijiandaa kuanza harakati za kumngoa madarakani kupitia bungeni.katika barabara za Harare kulikuwa na sherehe huku magari mengi yakipiga honi.
