Mwalimu mkuu amcharaza viboko mwalimu mwenzake.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Migango wilayani Biharamulo, amemchapa viboko mwalimu mwenzake mbele ya wanafunzi akimtuhumu kwa wizi wa sahani tano, pamoja na nusu kilo ya sukari iliyotolewa kwa ajili ya mahafali ya wahitimu wa darasa la saba.
Katika taarifa yake ya kulaani kitendo hicho, kaimu katibu wa Chama cha Walimu Tanzania CWT Wilaya ya Biharamulo Joseph Lugumba amesema kuwa, mwalimu mkuu Mateso Musaku alimpiga viboko mwalimu wake Hosea Masatu mbele ya wanafunzi, tukio ambalo linalaaniwa vikali.
Lugumba amesema baada ya kupata taarifa za mwalimu huyo kuchapwa viboko uongozi wa CWT ulifika shuleni hapo kujiridhisha, ambako wanafunzi na wazazi walithibitisha tukio hilo, ikidaiwa kwamba mwalimu huyo alifungwa kamba kwenye mti.
Amesema mwalimu Masatu alidaiwa kuiba vitu hivyo siku moja baada ya kumalizika mahafali ya darasa la saba, na kwamba alipoulizwa alikiri.

Exit mobile version