Mwanafunzi Aliyesambaza Picha za Nyufa Hostel za UDSM Aachiwa.

In Kitaifa

Mbunge wa serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Daruso), Kumbusho Dawson ameachiwa baada ya kuhojiwa na polisi wa kitengo cha makosa ya mtandao.

Kumbusho alipelekwa Kituo Kikuu cha Polisi jana Jumanne Desemba 5,2017 akitokea Oysterbay alikokwenda kuripoti asubuhi baada ya kuachiwa kwa dhamana juzi usiku.
Wakili Alex Masaba anayewakilisha Kumbusho amesema polisi wamemuachia baada ya mahojiano na wanaendelea na upelelezi hivyo wakimuhitaji watamwita.
Masaba amesema mteja wake alikamatwa kwa kosa la kusambaza picha zinazoonyesha nyufa kwenye jengo la mabweni ya chuo hicho. Hata hivyo, amesema anaamini kilichofanyika si jinai.
“Kosa la kusambaza picha zilizopigwa si jinai hata polisi nimewaeleza kwa kitendo kilichofanyika inabidi apongezwe,”amesema Masaba.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alieleza kuwa polisi ilimkamata na kufanya mahojiano na mwanafunzi huyo ili kujua lengo hasa la yeye kusambaza picha hizo pasipo kutoa taarifa kwa wamiliki wa majengo pamoja na wakala wa majengo husika.

“Huyo mwanafunzi alikamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi lakini alihojiwa na kuachiliwa kwa dhamana.

“Kilichopelekea akamatwe ni ule uzushi awa kuzunguka kwenye kwenye mitando.
“Sisi tulikuwa tunakitegemea kama angekuwa na taarifa yoyote, wamiliki wa majengo wapo, mkandarasi aliyefanya kazi ile yupo, kwa hiyo mtu ambaye angepaswa kuwa wa kwanza kulalamika angekuwa ni mmiliki wa majengo na sio yeye.
“Sasa yeye amefikia mahali akarusha, sijui alikuwa na maana gani, hatujaielewa vizuri..,” alisema Kamanda Mambosasa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu