Mwanaharakati aliyekamatwa kwa kumuita Rais Museveni “JOZI YA MAKALIO”hatimae apewa dhamana.

In Kimataifa

Mwanaharakati msomi nchini Uganda ambaye alikamatwa baada ya kumuita Rais Yoweri Museveni “jozi ya makalio”, hatimaye amepewa dhamana.

Dkt Stella Nyanzi alifikiwa mahakamani akionekana dhaifu.

Mwandishi wa BBC Patience Atuhaire aliyekuwepo kortini anasema mwanaharakati huyo alizirai alipojaribu kusimama baada ya kikao cha mahakama kuahirishwa kwa muda.

Alisaidiwa kusimama na maafisa wa magereza.

Taarifa zinasema anaugua Malaria.

Upande wa mashtaka ulikuwa umesema iwapo Dkt Nyanzi angepewa dhamana, basi mahakama iweke sharti kuwa achunguzwe afya yake ya kiakili.

Kadhalika, walitaka azuiwe kuandika au kuzungumzia chochote kuhusu Rais, serikali au familia ya Rais.

Mawakili wake hata hivyo walisema anafaa kupewa dhamana kutokana na hali yake ya afya na kwamba anafaa kuruhusiwa kupata nyaraka muhimu kuhusu kesi yake ili kujiandaa kujitetea.

Hakimu aliamua Dkt Nyanzi hafai kujihusisha katika shughuli zozote ambazo zinaweza kuingilia kesi hiyo dhidi yake.

Dkt Nyanzi alikamatwa mwezi Machi baada ya kuandika msururu wa ujumbe kwenye Facebook, ambapo alimshutumu rais Museveni kwa kushindaa kuwapa wasichana kutoka familia maskini vitambaa vya kutumia wakati wa hedhi.

Wasichana wengi nchini Uganda wameripotiwa kuacha masomo kutokana na aibu ya kukosa sodo.

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Maagizo ya wizara kuhusu mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikaliimeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo yakilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto

Read More...

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia. Akithibitisha

Read More...

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawaameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6ikiwa ni makadirio ya mapato

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu