Mwanajeshi aliyeuawa katika shambulio la kombora nchini Mali ametambuliwa leo ni mwanajeshi kutoka Liberia.

  Mwanajeshi wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa aliyeuwawa katika shambulio la kombora lililodaiwa na muungano wa wapiganaji jihadi nchini Mali ametambuliwa leo na umoja huo kuwa ni mwanajeshi kutoka Liberia.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaofahamika kama MINUSMA uliwekwa katika nchi hiyo ya Afrika magharibi tangu mwaka 2013 na unachukuliwa kuwa ujumbe hatari kabisa wa umoja huo unaofanyakazi ya kulinda amani.

Ujumbe huo wa MINUSMA umesema wanajeshi wengine wanane walijeruhiwa na shambulio hilo la kombora katika kambi yao katika mji wa kihistoria wa Timbuktu Jumatano mchana.

Liberia ina wanajeshi 78 wanaotumikia katika kikosi chenye wanajeshi 13,000 wa MINUSMA ambacho kinasaidia majeshi ya Mali yanayojaribu kuweka usalama nchini humo.

 

 

Exit mobile version