Mwanamke aliyepigwa picha akiuonyesha msafara wa rais Donald Trump ishara ya kidole cha kati ameripotiwa kufutwa kazi na kampuni iliomuajiri kufutia picha hiyo.
Picha hiyo ilisambazwa baada ya kupigwa mnamo terehe 28 mwezi Oktoba mjini Virginia karibu na uwanja wa kucheza Gofu wa Trump.
Juli Briskman ambaye alitambulika kama mwendesha baiskeli anadai kwamba alifutwa kazi na mwajiri wake Akima LLC baada ya kuichapisha katika mtandao wake.
Kampuni hiyo hatahivyo haikutoa tamko lolote ilipotakiwa kufanya hivyo na BBC.
Bi Briskman aliambia vyombo vya habari kwamba kampuni hiyo ilimuita katika mkutano siku moja baada ya kumwambia afisa mkuu wa ajira kwamba ni yeye ndiye aliyepiga picha hiyo.
