Aaron Joel mwenye miaka 42 huko Nevada amekimbilia ndani ya moto kwenye Burning man Festival na kisha kupata majeraha mabaya sana.
Watu walifanikiwa kumuokoa na kumkimbiza ndani ya hospital ya UC Davic huko Califonia,lakini kwa bahati mbaya umauti ulimpata.
Daktari walisema mwanaume uyo hakuwa ametumia kilevi chochote, na wanashangaa kwanini aliamua kuingia kwenye moto ule.
Kwa sasa wanaendelea kufanya uchunguzi kujua ni nini kilipelekea mwanaume huyo kufanya hivyo.
Waandaaji wa Festival hiyo ambayo inafanyika mara moja kwa mwaka, ambapo wanachoma mtu aliyetengenezwa kwa kutumia mbao na waandaaji, wamesema sio mara ya kwanza kitendo kama cha Aaron kutokea, kwani wale watu wanaohudhuria wamekua wakitaka kuingia ndani ya moto huo na wengine kufanya kama ukumbusho .
