Mwendesha mashtaka wa kesi za ufisadi nchini Brazil amfungulia mashtaka rais.

Mwendesha mashtaka wa kesi za ufisadi nchini Brazil amemfungulia mashtaka rais Michel Temer kwa kosa la kuzuia sheria kuchukuwa mkondo wake na kuhusika katika mtandao wa rushwa.

Hatua hiyo ni ya pili katika kesi ya jinai inayomkabili rais huyo ambaye amekanusha madai hayo.

Wanamtuhumu bwana Temor kwa kuchukua hongo na kujaribu kuwanyamazisha mashahidi.
Bwana Temer amepinga madai ya kufanya makosa yoyote.

Mashtaka ya awali ya ufisadi yalizuiwa na bunge la uwakilishi ambalo lina uwezo wa kuamua iwapo rais anafaa kufunguliwa mashtaka au la.

Katika shtaka la pili rais Temer ameshtakiwa pamoja na washirika wake sita wa kisiasa.

Kiongozi wa mashtaka Rodrigo Janot amesema katika taarifa kwamba bwana Temer alihudumu kama kiongozi wa genge la wahalifu linaloshirikisha wanachama waandamizi wa chama chake cha PMDB.

Exit mobile version