Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu, amesema wabunge ambao ni wajumbe kutoka kamati saba za Bunge wameridhia kuunda Chama cha Wabunge wanaotetea usalama barabarani endapo Spika wa Bunge ataridhia.

In Kitaifa

MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu, amesema wabunge ambao ni wajumbe kutoka kamati saba za Bunge wameridhia kuunda Chama cha Wabunge wanaotetea usalama barabarani endapo Spika wa Bunge ataridhia.

Balozi Adadi ambaye pia ni Mbunge wa Muheza na aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkutano huo ameyasema hayo jana mjini Dodoma, katika kilele cha Maadhimisho ya Nne ya Umoja wa Mataifa ya Wiki ya Usalama Barabarani ambayo kaulimbiu yake ilikuwa “Udhibiti wa Mwendokasi kwa Vyombo vya usafiri”.

Wabunge katika kamati zao saba wamefikia hatua hiyo zikiwa ni siku chache tangu kutokea ajali mkoani Arusha, iliyowaua wanafunzi 33 wa darasa la saba, walimu wawili na dereva wa Shule ya Msingi ya St. Lucky Vincent, wakati wakienda Karatu kufanya mtihani wa ujirani mwema kujipima na kujiandaa kwa mtihani wa mwisho.

Balozi Adadi amesema kwa siku mbili Mtandao wa Wadau kutoka Asasi za Kiraia unaotetea Marekebisho ya Sheria na Sera, inayohusu Usalama Barabarani nchini walikutana na kamati hizo kuzungumza na kujadili hali ya usalama barabarani ,na ikabainika kuwa, chanzo kikubwa cha matukio ya ajali za barabarani ni makosa ya kibinadamu.

Aidha, alisema wanaendeleza mtandao wa wabunge wanaotetea usalama wa barabarani ambao hadi sasa wapo 80 ili waweze kuingia kwenye mtandao wa wabunge wa dunia wa masuala ya usalama barabarani wakiwa na jukumu la kuhamasisha jamii kuhusu usalama sambamba na kuziangalia sheria za usalama barabarani kama zinakidhi. Kuhusu matatizo ya usalama barabarani, Balozi Adadi alisema mengi yamechangiwa na sababu za kibindamu ukiwamo uzembe wa madereva.

Alisema tafiti zinaonesha kwamba, asilimia 76 ya ajali zote zinatokana na vyanzo vya kibinadamu ikiwemo ulevi, mwendokasi, uzembe, uchovu, kupuuzia au kutokuwa makini wawapo barabarani pamoja na kutokutii sheria za usalama barabarani.

Mratibu wa Kitengo cha Usuluhishi wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Gladness Munuo alisema kwa mujibu wa ripoti ya Haki za Binadamu kwa mwaka 2016, ajali za barabarani zilipungua katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016, ikilinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2015.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu