Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba amewataka wananchi wa jimboni la Iramba Magharibi, wa jamii ya kifugaji kuachana na tamaduni za kutowapeleka watoto shule na kuwatumikisha kufuga mifugo yao.
Akizungumza wakati ziara yake jimboni Mwigulu amesema kuwa Urithi ulio mkubwa zaidi kwa mtoto ni Elimu,ambayo itamasaidia mtoto kwa maisha yake ya baadae.
Nchemba amezitaka jamii hizo kuachana na tamaduni ambazo zimepitwa na wakati kwani hali ya maisha imebadilika tofauti na miaka iliyopita.
Aidha amewataka kufuga kisasa kwa tija zaidi tofauti na hapo awali kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanasababisha ukame hivyo amewaasa kuwekeza katika elimu kwa kuwapeleka watoto shule ili waje kuwa msaada kwa baadaye.
Hata hivyo, katika ziara yake hiyo ya jimboni kwake, Nchemba ametembelea ujenzi wa hosteli katika kila shule ya Sekondari katika Kata 20 na kujionea maendeleo ya ujenzi huo ambao unaendelea kwa kasi kubwa
