Amesema nchi hiyo kwa sasa ina serikali ambayo inaweza kuaminika na mipango yenye maana.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Jumuia ya Kimataifa ina nafasi kubwa kuisaidia Somalia.
Hata hivyo Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo ameonya kuwa mapambano dhidi ya wapiganaji wa Al Shabaab yanaweza kuendelea kwa miongo kadhaa iwapo vikwazo vya silaha havitaondolewa.
Mkutano huo wa siku moja ulizungumzia pia tatizo linaloikabili Somalia la athari za ukame ambazo zinageuka kuwa baa la njaa.
