Naibu Meya wa Jiji la Arusha Mhe.Viola Likindikoki leo Oktoba 24 amefunga mafunzo ya kisheria katika kata ya Moivaro kwa kuwatunuku vyeti wanawake wajane wanaotoka ndani na nje ya kata ya Moivaro pamoja na watoto yatima wanaotoka katika kituo cha Tumaini vocetion training center.
Mafunzo hayo ya kisheria yaliandaliwa na Bi.Judy Owens na kufanyika katika kanisa la International evangelist Church,Pia Bi.Judy ndiye alikua Mkufunzi katika mafunzo hayo.Hata hivyo Mawakili walialikwa ili kutoa somo la kisheria katika mafunzo hayo,miongoni mwa mawakili walioalikwa ni Bi.Winniefrida Manyanga na Baraka Joel.
Mafunzo hayo ya kisheria yalifunguliwa miezi mitatu iliyopita na Diwani wa kata hiyo Mhe.Rick Moiro.
Wanawake hao wajane waliopokea Mafunzo hayo ya kisheria wametakiwa kwenda kuwafundisha wanawake wengine wajane wanaokaa ndani na nje ya kata hiyo waliokosa fursa ya kupata mafunzo hayo.
