Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe David Silinde
amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma Vijijini
Mkoa wa Mara, Msongela Palela kuhakikisha mpaka ifikapo
mwisho wa mwezi Desemba, mwaka huu awe amemaliza ujenzi
wa maabara katika shule mpya ya sekondari katika Kata ya
Ifulifu ambayo walipewa milioni 470 ya ujenzi, lakini mpaka
kufika leo hii fedha hizo zimekwisha huku maabara hizo zikiwa
bado hajimalizwa ujenzi wake.
Maagizo hayo ameyatoa akiwa katika ziara ya ukaguzi wa
ujenzi wa madarasa mapya mkoani humo na kukuta ujenzi wa
madarasa katika Wilaya ya Musoma ukiendelea vizuri na kutaka
wakamilishe kwa wakati ili kuruhusu wanafunzi wapya wa
kidato cha kwanza waweze kuingia mapema mwakani katika
mwaka mpya wa masomo Januari.
