Naibu waziri wa fedha na mipango Ashatu kijaji anatarajiwa kufungua mkutano wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya mstaafu (GEPF) utakaofanyika may 25 jijini Arusha.

In Kitaifa

Naibu waziri wa fedha na mipango  Ashatu kijaji anatarajiwa kufungua mkutano wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya mstaafu (GEPF) utakaofanyika may 25 jijini Arusha.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, Daudi Msangi amesema kuwa, mkutano huo utashirikisha wadau zaidi ya mia tatu kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini.

Amesema kuwa,katika mkutano huo wanatarajia kujadili Mada mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa wanachama pamoja na kuwasilisha taarifa za utendaji Kwa mwaka 2015/2016.

Msangi ameongeza kuwa, ndani Ya siku hizo mbili za mkutano mbali na kujadili taarifa za wanachama wanatarajia kutoa misaada wa mashuka Kwa watoto na wanawake wajawazito katika hospital ya dareda iliyopo wilayani babati Mkoani Manyara.

Hata hivyo ameongeza kuwa, mfuko huo umekuwa ukitoa misaada Kwa kuangalia mahitaji ya jamii popote nchini na kuweza kusaidia kulingana na mahitaji hayo.

Mwenyekiti wa bodi Ya wadhamini, Joyce shaidi amesema kuwa, mfuko huo unatarajia kuwekeza kiasi cha kiasi cha shs bilioni moja na milioni mia sita katika kiwanda cha kutengeneza mashine cha Kilimanjaro machine tools kilichopo Mkoani kilimanjaro Kwa ajili ya kujenga kinu kidogo cha kufua vyuma.

Amesema kuwa,uwepo wa kinu hicho utasaidia kuinua uzalishaji wa kiwanda hicho, huku kwa sasa watawekeza kinu kidogo ambapo kwa baadaye wataendelea na kuwekeza kinu kikubwa.

Kwa upande wa meneja masoko, Edgar shumbumbu amesema kuwa, mfuko huo unalenga zaidi kutumia radio za jamii katika kuwafikishia wananchi wa vijijini elimu ambapo wamepata mafanikio makubwa Sana kupitia mfumo huo.

Ameongeza kuwa, mfuko huo umekuwa ukitoa mafao mbalimbali ikiwemo fao la msaada wa mazishi Kwa wanachama wake, na sambamba na kutoa elimu kwa watoto wa wanachama.

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu