NAIBU WAZIRI WA MADINI, STANSLAUS NYONGO AANZA ZIARA YA SIKU MBILI TANGA

Leo tarehe 25 Juni, 2020 Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ameanza ziara ya siku mbili katika mkoa wa Tanga yenye lengo la kukagua shughuli za madini pamoja na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wachimbaji wa madini.

Mara baada ya kuwasili mkoani Tanga amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela.

Akizungumza kabla ya kuanza kwa ziara hiyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella mbali na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta ya Madini amesema kuwa ofisi yake imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga kwenye utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikumba Sekta ya Madini katika mkoa wa Tanga.

Exit mobile version