Naibu waziri wa nishati na madini Mhe. Dk. Medard Kalemani ameliagiza shirika la ugavi wa umeme nchini (TANESCO ) mkoani Mwanza kuhakikisha kuwa wateja ambao bado hawajaunganishiwa huduma hiyo, wanapatiwa umeme mara moja kabla ya julai 25 mwaka huu.
Dk. Kalemani ametoa agizo hilo wakati akizindua mradi wa kusambaza umeme vijijini ( REA ) awamu ya tatu katika mkoa wa Mwanza uliofanyika katika kijiji cha Nyamatala kata ya Ngulla wilayani Kwimba.
Mkurugenzi mkuu wa wakala wa umeme vijijini Mhandisi Gissima Nyamhanga, anasema mkandarasi wa mradi huo white city international inayoshirikiana na kampuni ya kichina iitwayo Gwadongi imepangiwa kutekeleza mradi huo katika vijiji 152 katika awamu ya kwanza inayoanza sasa hadi machi 2019.
Baadhi ya wabunge wa mkoa wa Mwanza, wakiongozwa na mbunge wa jimbo la Sumve Mhe. Richard Ndassa wamezungumzia changamoto za upatikanaji wa umeme zinazowakabili wananchi wa vijijini,
Aidha mkuu wa mkoa huo John Mongella amesema kuwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya juu wanatakiwa kusimamia mradi huo.
