Naibu waziri wa Utalii na Maliasili atoa rai kwa vyombo vya habari vyote Nchini.

Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani ametoa Rai Kwa vyombo vya habari vyote nchini kuwa na uzalendo wa kutangaza utalii wa ndani kwa nguvu zote na kupeleka ujumbe kwa watanzania wa kuhakikisha rasilimali asili ambazo ni vivutio vya utalii zinatunzwa na kuhifadhiwa kama urithi wa Taifa.

Mhandisi Makani akiwa katika hifadhi ya taifa ya Serengeti amesema Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi vya asili ikiwemo hifadhi ya taifa ya Serengeti na kwa maana hiyo ni muhimu rasilimali hizo zikatunzwa vilivyo kwa manufaa ya taifa na vizazi vijavyo.

Paschal Shelutete ni meneja mawasiliano wa shirika la hifadhi za taifa TANAPA anawahakikishia wanahabari kuwa ,shirika hilo linatambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kukuza utalii wa ndani na hata ule wa kimataifa na hivyo watahakikisha wanafanya kazi bega kwa bega na vyombo hivyo ili kuongeza uelewa wa dhana nzima za utalii wa ndani kwa watanzania wote,huku muhifadhi wa Serengeti William mwakilema akikiri kuwa utalii mpaya wa balloon umechangia ongezeko la watalii .

Hifadhi ya taifa ya Serengeti ni moja kati ya hifadhi maarufu sana duniani. Umaarufu wa hifadhi hii unatokana na misafara mirefu ya nyumbu wanao hama kwa makundi makubwa kutoka upande mmoja wa mbuga hadi mwingine, na kuvuka mpaka wa Tanzania hadi hifadhi ya taifa ya maasai mara nchini Kenya.

Exit mobile version