Nana Akufo-Addo achaguliwa tena kuwa rais wa Ghana

In Kimataifa

Rais Nana Akufo Addo, wa Ghana ameshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, kwa kupata asilimia 51.6 ya Kura, dhidi mpinzani wake wa karibu, Rais wa Zamani wa taifa hilo, John Mahama aliyepata asilimia 47.4 ya kura zote.

Mwenyekiti wa Tume ya taifa ya Uchaguzi Ghana, Jena Mensa, ndiye aliyetangaza matokeo mjini Accra

Rais Akufo Addo ametetea nafasi yake hiyo,dhidi ya mpinzani wake huyo ambaye tangu awali alionyesha wasiwasi wake wa kutumika kwa nguvu ya Jeshi kwenye uchaguzi huo.

Bwana Mahama amelalamikia wizi wa kura. Akiongea muda mfupi baada ya tangazo hilo, Rais Akufo Addo amewashukuru raia kwa kumchagua.

“Nimeguswa tena sana na kuaminiwa nanyi na sichukulii hili kuwa jambo dogo…labda ipo tabia ya kuwa rais aliyepo madarakani akichaguliwa tena muhula wa pili anachukulia hilo kiurahisi na kuanza kupumzika …lakini mimi ni wa tofauti.

Ninawashukuru sana , Waghana wenzangu kwa ushindi huu”.

Ingawa Mahama hajakubaliana na matokeo hayo.

Hii ni mara ya pili kwa wapinzani hawa wa kisaiasa kukabiliana katika uchaguzi mkuu wa rais.

Ghana inasifika kuwa taifa lenye demokrasia barani Afrika.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TEMBO WAUA TENA KIGONIGONI

Aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Kigonigoni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Yonael Kaindu Maarufu kama Mzembi, ameshambuliwa na Kuuawa na

Read More...

Waziri wa zamani wa Msumbiji ahukumiwa kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi.

Msumbiji Alhamisi imemuhukumu waziri wa zamani kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi, ikiwa ni hukumu kali

Read More...

YANGA yasaini Mkataba mpya wa Udhamini na Sportpesa

KLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu