Nape: Nitashugulika na CCM bila kutoka.

In Kitaifa, Siasa

Mbunge wa Jimbo la Mtama (CCM) Nape Nnauye amesema kuwa tetesi zilizokuwa zikizagaa na kuzungumzwa kuwa naye yuko mbioni kuhama chama chake cha mapinduzi kama ambavyo amefanya Lazaro Nyalandu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha wakiwa watatu akiwemo yeye, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, na aliyekuwa Mbunge kupitia CCM ambaye amejivua uanachama Lazaro Nyalandu.

Aidha Nape ameandika maneno ambayo yanaonyesha hana mpango wa kuhama chama chake kama ambavyo inahisiwa na watu mbali mbali, lakini akasema atainyoosha CCM akiwa ndani ya chama hicho.

“Chama cha siasa ni itikadi, itikadi ni imani.Siamini sana katika kubadili imani kienyeji.Nitashughulikia mapungufu nikiwa ndani na sio nje ili kukiweka sawa chama kinapoyumba na si vingine,”ameandika Nape
Kufuatia kuonyesha msimamo huo, hii moja kwa moja itafunga majadiliano ya watu katika sehemu tofauti kuwa ana mpango wa kukitosa Chama cha Mapinduzi c CCM.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Maagizo ya wizara kuhusu mfuko wa maendeleo ya kilimo.

Naibu Waziri Wa Kilimo Anthony Mavunde, amesema serikaliimeanza kutekeleza uanzishwaji wa mfuko wa maendeleo yakilimo utakaosaidia kukabiliana na changamoto

Read More...

TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia. Akithibitisha

Read More...

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Professor Makame Mbarawaameliomba Bunge kumuidhinishia kiasi cha Sh Trilioni 3.6ikiwa ni makadirio ya mapato

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu