Nasa waenda Mahakamani kupinga matokeo ya urais.

Uongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa nchini Kenya, umeamua kwenda Mahakama kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu, yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta.

Kwa uamuzi huo Rais Kenyatta hataapishwa tena Agosti 29 kama ilivyotarajiwa, kwani atatakiwa kusubiri hatima ya kesi hiyo, ambayo inapaswa kusikilizwa kwa muda usiozidi siku 14.

Ikiwa Mahakama ya Juu nchini humo itatupa kesi hiyo,Kenyatta ataapishwa Septemba 12, lakini ikiwa ushahidi utaonyesha wizi Wakenya watarudi katika uchaguzi.

Msimamo wa Nasa kwenda kortini umekuja siku chache, baada ya Rais Kenyatta kumtaka Odinga asitumie njia zinazoweza kusababisha machafuko, bali kwenda mahakamani kupata haki yake.

 

 

 

 

 

Exit mobile version