NATO yatishia kuishambulia Korea Kaskazini.

 

 

Katibu Mkuu wa Shirika la kujihami la nchi za magharibi NATO Jens Stoltenberg, amesema mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini ni tisho kwa usalama wa dunia nzima, na kama zisipochukuliwa hatua stahiki basi kuna uwezekano wa kuleta madhara makubwa.

Amesema katika sheria ambazo shirika limejiwekea, ni pamoja na ile inayosema kuwa mwanachama mmoja akishambuliwa basi itakuwa limeshambuliwa shirika zima, hivyo kutanabaisha kwa kile kinachoendelea Korea Kaskazini.

Aidha alipoulizwa kama shirika hilo lina mpango wa kuishambulia Korea Kaskazini amesema kuwa, hana uhakika kama watatumia sheria hiyo, inayosema mwanachama mmoja akishambuliwa basi shirika zima limeshambuliwa.

Hata hivyo ametoa wito kwa Korea Kaskazini kuacha mpango wake wa kutengeneza silaha za nyuklia, huku akisema kufanya hivyo ni ukiukwaji mkubwa wa maazimio ya Umoja wa Mataifa na ni tishio kwa amani ya dunia.

Exit mobile version