Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki
Profesa Palamagamba John Kabudi amesema,uchaguzi wa
mwaka huu utakuwa na waangalizi kutoka mataifa 15.
Mbali na waangalizi kutoka katika nchi hizo pia waziri Kabudi
ameeleza kuwa uchaguzi wa mwaka huu unagharamikiwa na
serikali kwa asilimia mia moja bila fedha kutoka nchi za nje.
