NCHI za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania zinawasilisha bajeti zao kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

In Kitaifa

NCHI za Afrika Mashariki ikiwamo Tanzania zinawasilisha bajeti zao kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango anatarajiwa kuwasilisha bajeti hiyo bungeni leo mjini hapa kuanzia saa 10 kamili jioni.

Kabla ya kufanya hivyo, asubuhi Dk Mpango atawasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi ya nchi, ambayo itajikita katika kueleza mipango ya maendeleo kwa mwaka ujao.

Kwa mujibu wa ratiba ya Bunge la Tanzania katika Mkutano wake wa Saba wa Bunge la Bajeti, wabunge watatumia kesho kusoma na kutafakari hotuba hiyo.

Kuanzia Jumatatu ijayo Juni 12 hadi Juni 20, mwaka huu, wabunge watajadili Taarifa ya Hali ya Uchumi na Bajeti ya Serikali kwa siku saba kabla ya jioni ya Juni 20, mjadala kuhitimishwa kwa upigaji kura ya wazi.

Machi 29, mwaka huu, Dk Mpango alisoma bungeni mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na kiwango cha ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa 2017/18, na kueleza kuwa serikali katika bajeti hiyo inatarajia kuwa na ukomo wa Sh trilioni 31.6.

Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 inayomalizika Juni 30, mwaka huu ilikuwa ya Sh trilioni 29.5. Katika Sh trilioni 31.6, za maendeleo zimeongezeka kutoka Sh trilioni 11.8 katika mwaka 2016/17 hadi Sh trilioni 11.9 katika mwaka wa bajeti 2017/18.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

RC MBEYA AFANYA UZINDUZI ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA (NIDA)

Mkuu wa mkoa wa mbeya Mhe. Comrede Juma Zuberi Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho

Read More...

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu