Ndalichako asema uhakiki wa vyeti feki ulifanyika kwa umakini na kwa uhakika ili kutenda haki.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo wa Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema uhakiki wa vyeti feki ulifanyika kwa umakini na kwa uhakika ili kutenda haki.

Ripoti iliyokabidhiwa kwa Rais John Magufuli na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Angela Kairuki, ilikuwa na orodha ya watumishi wa umma 9,932 walionainika kuwa na vyeti feki. Profesa Ndalichako alisema hadi kufikia kuwaweka wazi, ulifanyika uchunguzi wa kina na makini.

Amesema baada ya uhakiki huo uliojikita katika vyeti vya kidato cha nne, kidato cha sita na ualimu, zamu inayofuata ni uhakiki wa vya kitaaluma baada ya kukamilika kwa uhakiki wa watumishi wa Serikali Kuu utakaotangazwa wiki hii.

Amesema Serikali imeziba njia zote za mkato katika elimu na ajira hivyo, vijana watumie muda walio nao kusaoma kwa bidii. Aliwataka waliojiunga katika vyuo vikuu bila sifa stahiki kuwajisalimishe ili kuepuka majuto ya baadaye.

Profesa Ndalichako alisema suala la kughushi vyeti vya taaluma na kutumia vya wengine limekuwa changamoto kubwa nchini.

Ndalichako amesema  serikali ina dhamira ya kuhakikisha watumishi wenye sifa stahiki wanakuwepo kwenye utumishi wa umma na si vinginevyo na kwamba, Mei 5, mwaka huu Serikali itatoa taarifa ya uhakiki wa watumishi wa Serikali Kuu.

Exit mobile version