Spika wa Bunge , Job Ndugai amemtimua bungeni mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuvaa suruali inayombana.
Mbunge huyo wa Momba Condester Sichwale alitimuliwa bungeni na Spika, kulingana na kanuni za Bunge, ambazo zinawataka wabunge wanawake kutovaa suruali za kubana.
Hatua ya kufukuzwa bungeni kwa Mbunge Sichwale imekuja baada ya mbunge wa CCM wa Nyang’wale Hussein Amar kusimama na kuomba mwongozo wa Spika, huku akisema kuwa kuna wanawake waliokiuka kuvaa mavazi ya staha.
Spika Ndugai alimpa nafasi mbunge huyo kumtaja mwenzake aliyevaa mavazi ambayo hayakuwa na staha ili iwe mfano na ndipo alipoashiria alipokaa mbunge huyo bila kumtaja jina.
Hatahivyo Spika alisimama na kumtaka mbunge aliyevaa mavazi hayo asimame na aondoke ndani ya ukumbi ili akavae mavazi yenye staha ndipo atarejea tena bungeni.