Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imesema wakati wowote kuanzia leo Jumatatu, itaeleza kinachoendelea kuhusu kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa Jimbo la Singida Kaskazini.
Jimbo hilo liko wazi tangu Oktoba 29 mwaka huu, baada ya aliyekuwa mbunge wake kupitia CCM Lazaro Nyalandu kujiuzulu uanachama wa chama hicho.
Akizungumza na wanahabari Mkurugenzi wa Uchaguzi Ramadhan Kailima amesema kuwa, muda si mrefu watatoa taarifa ya kinachoendelea.
Kuhusu hatima ya waliokuwa wabunge nane wa CUF ambao hivi karibuni Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewarejeshea uanachama, Kailima amesema wao wanapokea maagizo kutoka kwa mamlaka husika, na mpaka sasa bado hatujapokea.
