Neema Kuwashukia wafanyakazi wa Manyumbani.

Serikali imetakiwa kuridhia na kupitisha mkataba wa kimataifa wa wafanayakazi wa majumbani namba 189 wa kazi zenye staha wa mwaka 2011 ili kuwezesha haki za wafanyakazi wa majumbani zifatwe kisheria.
Mkataba wa wafanyakazi wa majumbani ulipitishwa tarehe 16/6/2011 na shirika la kazi duniani ILO huko Geneva Switzerland ambapo hadi sasa aslimia kubwa ya nchi hazijaridhia  mkataba huo ikiwemo Tanzania.
Hata hivyo katika kuadhimisha siku ya wafanyakazi wa majumbani Watanzania wameungana na mataifa mengine duniani katika maadhimisho hayo ambapo endapo mkataba huo utaraidhiwa utakuwa ni suluhisho kwa matatizo ya wafanyakazi.
Akizungumza na wafanyakazi wa majumbani Mwenyekiti wa wanawake kutoka chama hicho Atupaksye Mtafya amesema kuwa endapo mkataba huo utaridhiwa na kupitishwa itakuwa chachu ya mabadiliko kwa wafanyakazi wa majumbani ikiwemo kupata haki zao za msingi .
Nao baadhi ya wafanyakazi wa majumbani  wameiomba serikali kuitambua rasmi kada hiyo katika kuchochea uchumi wa nchi huku wakieleza changamoto wanazokumbana nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao
Exit mobile version