NEMC yapewa siku 7 kukifunga kiwanda cha ANBANGS kwa kukaidi maagizo ya serikali ya awamu ya tano.

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limepewa siku saba kukagua na kujiridhisha na uzalishaji na utekelezaji wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 ,na kanuni zake kwa Kiwanda cha ANBANGS kinachotengeneza mifuko aina ya viroba vinavyotumika kama vifungashio vya saruji, sukari na aina nyingine ya nafaka, na kukifunga kwa kwa kukaidi  Maagizo ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kutokulipa faini kwa uchafuzi wa Mazingira.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira katika maeneo ya Sukita Mivinjeni Buguruni jijini Dar es salaam.
Aidha, Mpina amelitaka baraza hilo kupitia nyaraka zote muhimu zinazohusu kiwanda hicho ambacho awali hakikuwa na cheti ya tathmini, ya Athari za Mazingira wala vibali ya aina yoyote vya kutirirsha maji yaliyotibiwa na kuuganishwa na Mfumo wa maji Taka wa DAWASCO, hali ambayo iliyopelekea wamiliki wa kiwanda hicho kufikishwa mahakamani.
Aidha Mpina ameahidi kushirikiana na mamlaka husika kuchukua sampuli za maji yanayopita katika bonde la mto msimbazi katika eneo la viwanda, vya karibu na mtaa wa sukita mivinjeni, ili kuyafanyia vipimo na kujirisha kama yana madhara kwa viumbe hai na mazingira hususani mboga mboga zinazomwagiliwa maji katika maeneo.
Exit mobile version