Neymar arejea katika mji wa Barcelona.

 

Mshambuliaji wa klab ya PSG ya Ufaransa Neymar Jr, amerejea Barcelona na kujumuika na wachezaji kadhaa akiwemo Lionel Messi na Gerard Pique.

 

Neymar alikuwa jijini Barcelona nyumbani kwake, kusharekea siku ya kuzaliwa ya mwanaye Davi Lucca.

 

Wakati Neymar akiwa na Pique, Messi na Raktic kutoka FC Barcelona, saa moja baadaye klabu hiyo imetangaza kumshtaki kutaka ilipwe asilimia kumi tena ya pauni milini 198, baada ya Neymar kuhamia PSG ya Ufaransa.

 

Messi alitupia picha hiyo wakiwa pamoja wenye furaha kusherekea siku ya kuzaliwa ya Davi Lucca, na kusema “Hes is back”, yaani amerejea.

 

Neymar alisajiliwa na Paris Saint-Germain ya Ufaransa kwa dau la pauni 198 milioni, na kaovunja rekodi ya dunia akitokea Barcelona ya nchini Hispania mwishoni wa mwezi Julai mwaka huu.

Exit mobile version