NHC YATOA KIWANJA KWA JESHI LA POLISI ENEO LA SAFARI CITY.

In Kitaifa
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limetoa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 5000 kwa Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi na nyumba za askari katika eneo la Matevesi ambapo kuna mradi wa Safari City umbali wa kilomita 12 kutoka katya mji wa Arusha.
 
Akizungumza mara baada ya kukabidhi eneo hilo kwa Jeshi la Polisi, Mkuu wa Masoko wa Shirika hilo nchini Bw. Itandula Gambalagi alisema kwamba, wanatambua umuhimu wa Usalama ndio maana wameamua kutoa eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi pamoja na makazi ya askari.
 
Alisema uwepo wa Jeshi la Polisi katika eneo hilo utawavutia wawekezaji na wakazi wa eneo hilo kuwa na uhakika wa usalama wao na kuliomba Jeshi hilo kuanza kufanya maandilizi ya ujenzi wa kituo hicho kabla ya makazi na maeneo ya biashara hayajafunguliwa.
 
Akitoa shukrani zake kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema kwamba Jeshi hilo litachukua hatua za mapema ili kuweza kujenga kituo hicho ambacho kitaimarisha usalama katika eneo hilo.
 
“Watu wanaotaka kuwekeza katika eneo hilo wasiwe na shaka juu ya hali ya usalama lakini pia kituo hicho kitasaidia wakazi wa maeneo jirani na kiwanda cha A to Z kilichopo kilomita kadhaa kutoka katika kituo hicho”. Alisisitiza Kamanda Mkumbo
 
Naye Meneja Mradi wa Safari City Bw. James Kisarika alisema kwamba mbali na maeneo ya makazi pamoja na biashara lakini pia wametenga maeneo kwa ajili ya huduma za jamii kama vile viwanja kwa ajili ya ujenzi wa hospitali, Misikiti, Makanisa, Shule za Sekondari na Msingi, kituo cha mabasi madogo pamoja na viwanja vya Michezo.
 
Alisema kwamba mpaka hivi sasa tayari huduma za Maji na Umeme zinapatikana bila shaka yoyote na kuongeza kwamba miundo mbinu ya barabara ipo vizuri.
Picha no.1. Mkuu wa Masoko nchini wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Itandula Gambalagi akimkabidhi barua Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo ambayo inaelezea makabidhiano ya kiwanja toka Shirika hilo kwenda Jeshi la Polisi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi na makazi ya askari eneo la Matevesi ambapo ulipo mradi wa uwekezaji wa Safari City. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 
Picha no.2. Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kukabidhiwa eneo hilo na NHC kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi na makazi ya askari katika eneo la mradi wa Safari City, kushoto kwake aliyesimama ni Mkuu wa Masoko wa Shirika hilo Bw. Itandula Gambalagi (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)
 
Picha no.3. Baadhi ya viongozi wa NHC wakimuonyesha Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo mipaka ya kiwanja walichokikabidhi kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Polisi na makazi ya askari. (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Serikali kuunga mkono juhudi za Taasisi mbali mbali.

Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi, amesema serikaliitaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Taasisi yaZanzibar Maisha Bora Foundation,pamoja na

Read More...

DKT. KIRUSWA AZINDUA MFUMO WA USHIRIKISHWAJI WA WATANZANIA KATIKA SEKTA YA MADINI

Watanzania waendelea kunufaika Sekta ya Madini, ajira 15,341 zamwagwa, manunuzi ya ndani ya nchi yafikia Dola za Marekani bilioni

Read More...

MAFURIKO YAUWA 190 MALAWI

Takriban watu 190 sasa wamethibitishwa kufariki nchini Malawi baada ya Dhoruba ya Mafuriko ya Tropiki Freddy kulikumba eneo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu