Nusu ya Maiti 400 zazikwa Sierra Leone.

Wizara ya afya nchini Sierra Leone imesema kuwa, takriban nusu ya maiti 400 zilizotokana na maporomoko ya udongo na mafuriko, nje ya mji wa Freetown tayari zimezikwa.

Serikali ilisema mazishi ya pamoja yangefanyika leo, lakini mkuu wa wataalamu wa magonjwa kutoka mjini Freetown, amesema kwamba baadhi ya mazishi yalikuwa yamefanyika.

Imefahamika kuwa mazishi hayo yamehusisha miili ambayo, tayari ilitambuliwa au ilikuwa imeharibika vibaya.

Watu wapatao mia sita mpaka sasa, bado hawajulikani walipo.

Rais wa Sierra Leone ametangaza siku saba za maombolezi

Exit mobile version