Aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini CCM Lazaro Nyalandu, amesema ni kwa nini ameamua kutaka kujiunga chadema na sio chama kingine cha siasa hapa nchini.
Nyalandu ambaye amewahi kuwa naibu waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara na baadaye Maliasili na Utalii kabla ya kuwa waziri kamili, alitangaza uamuzi wa kuhama CCM Jumatatu.
Moja ya sababu alizozieleza ni kutoridhishwi na mwenendo wa kisiasa nchini, ukiukwaji wa haki za binadamu, dhuluma na mihimili miwili ya nchi kushindwa kufanya kazi yake kwa uhuru.
Amesema kuhama CCM ni kitu kilichomchukua muda mrefu, kutokana na yanayoendelea ndani ya chama hicho tawala,na hapa anaeleza kwa nini ameamua kuelekea CHADEMA.
Pia Nyalandu amesema uamuzi wake wa kujitoa CCM ni moja ya mambo matatu makubwa aliyofanya maishani hadi sasa.
Uamuzi wa kwanza ukiwa ni wa kumfuata Yesu Kristo awe mwokozi wa maisha yake, wa pili kuamua mwanamke gani awe mke wake na watatu ni huo wa kuamua kuachana na CCM.
