Obama ajitokeza kufanya kazi ya mzee wa baraza Chicago.

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alifika katika majengo ya mahakama moja Chicago kuitikia wito wa kuhudumu kama mzee wa baraza la mahakama.

Hata hivyo, jaji alimwamuru aondoke bila kuhudumu.

Umati wa watu ulikusanyika katika jengo la manispaa la Daley Center kumuona rais huyo wa 44 wa Marekani, ambaye ana nyumba katika jiji la Illinois.

Bw Obama aliondoka kwake nyumbani mwendo wa saa tatu unusu saa za huko siku ya Jumatano na aliondoka majengo ya mahakama saa sita hivi mchana.

Kila mtu aliyekabidhiwa wito wa kuhudumu kama mzee wa baraza mahakamani hupokea hundi ya $17.20 (£13.11) kutoka kwa wilaya hiyo.

Exit mobile version