Obama amkosoa Trump

In Kimataifa

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obam amemkosoa vikali Rais Donald Trump kwa namna anavyoshughulikia janga la corona.

Kauli yake ameitoa alipofanya mazungumzo na wafanyakazi wake wa zamani kuungana na timu ya kampeni ya uchaguzi ya Joe Biden, televisheni ya CNN imeeleza

Ikulu ya Marekani imejibu kuwa hatua ya Rais “isiyo ya kawaida” ilikuwa “imeokoa maisha ya Wamarekani”.

Wakati wa simu hiyo, Bw Obama alisema mbinu ya mrithi wake wa Republican kwa serikali ni sehemu ya kulaumiwa kwa namna alivyolishughulikia janga la corona.

Bwana Obama pia amekosoa vikali uamuzi wa kufuta mashtaka dhidi ya mshauri wa masuala ya usalama wa taifa Michael Flynn.

Zaidi ya watu 77,000 wamepoteza maisha na Marekani sasa ina wagonjwa milioni 1.2 wa virusi vya corona, takwimu hizo zote ni za juu zaidi ulimwenguni.

Nchi nyingi ziliweka marufuku ya kutotoka nje mwezi Machi, lakini masharti hayo sasa yameondolewa, na kuruhusu watu kurudi kwenye shughuli zao.

Lakini maafisa wa afya wanaonya kuwa hatua hii inaweza kusababisha virusi kusambaa zaidi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu