Paka mmoja nchini Uingereza aliyekuwa na mazoea ya kuiba
nguo na chakula mara kwa mara kutoka kwa majirani
amenaswa.
Mmiliki wa paka huyo Donna Hibbert, akiwa amejawa na soni,
ameingia kwenye mtandao wa Facebook akijaribu kurudisha
vitu hivyo.
Paka huyo kwa jina Harry, anaripotiwa kwamba amekuwa
akipeleka nyumbani mara kwa mara bidhaa zilizoibwa ikiwa ni
pamoja na nguo za ndani, pakiti ya soseji na hata kiatu cha
wabunifu katika kipindi cha miaka minne iliyopita.
Kulingana na Hibbert katika wiki moja iliyopita, Harry
alichukua vitu sita kutoka kwa majirani akifikiria ni zawadi.
Baadhi ya vitu hivyo vimechukuliwa kutoka kweny kamba za
kuanikia nguo,lakini vingine vimechukuliwa kutoka ndani ya
nyumba za watu.
Kaka yake Harry anaitwa Luna pia ni ,lakini kwa kawaida
huchukua vitu kama vile pakiti nyororo na pakiti za sigara.
Hibbert sasa ameanza kuchapisha vitu vilivyoibiwa kwenye
ukurasa wa Facebook wa Spotted,ambapo hata jirani wake wa
karibu ameweza kutambua vitu vyake.
