Papa Francis ameondoka Colombia akitoa miito ya maridhiano, baada ya nusu karne ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na kumalizika kwa amani kwa mzozo wa umwagaji damu katika taifa jirani la Venezuela.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani mwenye umri wa miaka 80, aliongoza misa kadha katika mji wa Cartagena, mojawapo ya vivutio muhimu kwa watalii.
Papa Francis aliitembelea wilaya masikini ya San Francisco, ambako alibariki msingi wa jengo jipya la watu wasio na makazi.
Papa Francis aliondoka Cartagena jana jioni, kurejea mjini Roma.