Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amekataa ushabiki na kutoa wito wa upendo katika misa iliyofurahiwa na umati wa maelfu ya Wakatoliki wa Misri wakati wa ziara inayolenga kuimarisha maridhiano na waislmu na kuwaunga mkono wakristo wachache nchini humo.
Ziara hiyo inayofanyika baada ya kundi la Islamic State kuwaua waumini kadhaa katika mashambulizi matatu kwenye makanisa mwezi Desemba mwaka jana na Aprili mwaka huu, imewapa wakristo hao wenye mazingira magumu ya kuabudu fursa ya kusherehekea.
Papa Francis amewaambia waumini kuwa ushabiki ambao waumini wanapaswa kuwa nao ni ushabiki wa upendo na ushabiki mwingine hautoki kwa Mungu.
Kiongozi huyo wa kiroho kwa karibu wakatoliki bilioni 1.3 duniani anakuwa papa wa kwanza kutembelea makao makuu ya imam mkuu wa Al-Azhar, Ahmed al-Tayeb, mmoja wa viongozi wa malaka ya juu ya kiislamu duniani.
