Mwanamke mmoja wa Canada alipata karoti ya ziada na pete ya almasi baada ya kupatikana katika shamba lake la mboga miaka 13 baada ya kuipoteza.
Mary Grams mwenye umri wa miaka 84, alipata shida alipopoteza pete hiyo wakati akipalilia shamba la familia mjini Alberta 2004.
Lakini alifanya kupotea kwa pete hiyo kuwa siri kwa takriban miaka 13.
Aliamua kutomwambia mumewe wakati alipoipoteza kwa kuona aibu, lakini alimwambia mwanawe.
Alienda kununua pete iliofanana na aliyopoteza na kuvaa na kuendelea kuishi kama ambaye hakuna kilichotokea.
Siku ya Jumatatu mkwe wake aligundua siri hiyo na pete hiyo baada ya kuvuna karoti moja.
Karoti hiyo ilikuwa imeota kupitia pete hiyo,na Bi Daley ambaye sasa anaishi katika shamba hilo aliona pete hiyo wakati alipokuwa akiosha karoti moja kubwa.
