Mshambuliaji wa klabu ya Stoke ya Uingereza Peter Crouch, ameingizwa kwenye kitambu cha rekodi za dunia cha Guinness World Records cha mwaka 2018 kwa kufunga mabao mengi zaidi kwa kichwa Ligi ya Uingereza.
Crouch amefunga mabao 51 kwa kichwa katika ligi hiyo, mabao matano zaidi ya mshambuliaji wa zamani wa Blackburn na Newcastle Alan Shearer.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amefunga jumla ya mabao 105 katika ligi kuu ya Uingereza katika mechi 436 alizochezea jumla ya klabu sita ligi hiyo.
Crouch alifunga bao la ushindi mechi ya karibuni zaidi ya Stoke walipocheza dhidi ya Southampton katika ligi kuu ya Uingereza.
