Polepole asema ccm sasa ni chama cha wananchi wote.

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amesema zama za watu wachache wenye fedha chafu, kuhonga wanachama na kuweka viongozi wanaowataka, zimekwisha.

Amesema CCM sasa ni chama cha wanachama wote kama Katiba inavyosema, bila ya kujali rika wala rangi na wenye kutaka uongozi ndani ya chama kwa kutumia fedha chafu, chama hakitasita kuwachukulia hatua ikiwamo kukata majina yao.

Kiongozi huyo wa CCM ameyasema hayo mkoani Arusha alipokutana na viongozi wa chama wa Wilaya ya Arusha ,kutoka kata zote 25 wakiwemo wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Arusha.

Aidha amewataka wanaCCM kuwataja viongozi wanaotaka uongozi ,kwa kugawa fedha chafu ili hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao.

Polepole amewataka wakazi wa Arusha kutorudia makosa yaliyojitokeza katika uchaguzi zilizopita.

Exit mobile version